MAN CITY ‘KUMDAKA’ KIPA WA BENFICA KWA DAU LA DUNIA!
City washaafikiana na Benfica kulipa Dau la Pauni Milioni 35 kumnunua Ederson mwenye Miaka 23.
Dili hii itamfanya Kipa huyo kutoka Brazil kuwa Kipa wa Bei Ghali mno katika Historia akivunja Rekodi ya Juventus ya Italy ya Mwaka 2001 ilipolipa Pauni Milioni 32.6 kumnunua Gianluigi Buffon kutoka Parma.
Jana Ederson alatajiwa kutua Jiji la Manchester ili kupimwa Afya yake na kisha kukamilisha Uhamisho wake ambao ni wa pili kwa city hivi sasa baada ya kumchukua Mchezaji wa Portugal Bernado Silva kutoka AS Monaco kwa Dau la Pauni Milioni 45.
ZA AWALI:
SILVA KUTUA CITY
Msimu
huu, Silva, mwenye Miaka 22, aliisaidia sana Monaco kutwaa Ubingwa wa
Ligi 1 huko France na pia kuifikisha Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI.
Silva ameichezea Timu ya Taifa ya Portugal mara 12 na kufunga Bao 1 na kukipiga Mechi 58 na Monaco akifunga Bao 11.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni