UEFA CHAMPIONZ LIGI - FAINALI - REAL v JUVE: BALE APOTEZA MATUMAINI, ISCO KUANZA?
UEFA CHAMPIONZ LIGI - FAINALI
Jumamosi Juni 3 Saa 3 Dak 45 Usiku
Millenium Stadium, Cardiff, Wales
Real Madrid v Juventus
××××××××××××××××××××××
Timu hizi zote zimemaliza Ligi zao kwa kutwaa Ubingwa wa Nchi zao
lakini Real wanatinga Fainali hii wakitaka kutetea Taji lao la UCL na
kuweka Rekodi ya kuwa Timu ya Kwanza kutenda hilo.
Kila Timu hivi sasa ipo kwenye maandalizi makali na huko Spain
umezuka mjadala mkali kuhusu nani aanze Mechi hii kubwa kati ya Gareth
Bale na Isco wa Real Madrid.
Kikawaida Bale ndie chaguo la kwanza la Kocha Zinedine Zidane na
Bale akicheza Mechi hii italeta shamrashamra kubwa humo Millenium
Stadium kwani humo ni Mtoto wa Nyumbani Cardiff ukiwa ndio Mji
aliozaliwa.
Lakini tatizo kubwa ni kuwa Bale alikuwa Majeruhi ingawa sasa yupo Mazoezini kama kawaida na wenzake.
Mwenyewe Bale amekiri kwamba ingawa yuko fiti itakuwa ngumu kwake
kuanza Fainali hii na matumaini ni kuwa ataingizwa toka Benchi.
Bale aliumia Enka yake Mwezi Novemba kwenye Mechi ya UCL dhidi ya
Sporting Lisbon na kuwa nje kwa Siku 88 na kurejea Uwanjani Siku Real
inacheza na Espanyol.
Pia alianza Mechi na Barcelona hapo Aprili 23 na kutoka nje Kipindi
cha Kwanza akiwa na maumivu ya Enka na tangu wakati huo hajacheza tena.
Kukosekana kwa Bale ndiko kulimpa nafasi Isco kung'ara Uwanjani.
Hata hivyo, Bale amesema ni juu ya Zidane kuamua nani amwanzishe na
ikiwa ni yeye yuko tayari kutimiza ndoto yake kucheza Fainali kubwa ya
Ulaya Nyumbani kwao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni