MANCHESTER UNITED NDIO KLABU YENYE THAMANI KUBWA ULAYA – KPMG!
Utafiti wa KPMG umeonyesha Man United, ambao ni Mabingwa wa UEFA EUROPA LIGI, wapo mbele ya Klabu Vigogo za Spain, Real Madrid na Barcelona wakiwa na Thamani ya Euro Bilioni 3.09.
Utafiti huo ulichunguza Haki za Matangazo na Mapato yatokanyo, Faida, Umaarufu, Uwezo Kimichezo na Umiliki wa Viwanja.
Utafiti huo ulipitia Mahesabu ya Klabu 32 huko Ulaya na 6 kati ya zile 10 Bora zinatoka England.
Mahesabu yaliyopitiwa ni yale ya Misimu ya 2014/15 na 2015/16.
Mkuu wa Michezo wa KPMG, Andrea Sartori, ambae ndie Mwandishi wa Ripoti ya Utafiti huu, amesema Kibiashara Sekta ya Soka imekua mno kwa Mwaka Mmoja uliopita.
Kuhusu Haki za Matangazo, Sartori amesema England inaongoza kwa mbali mno kwenye Mapato ya eneo hili.
+++++++++++++++++++++
10 BORA kwa Thamani Ulaya:
Manchester United – Euro Bilioni 3.09
Real Madrid - 2.97
Barcelona - 2.76
Bayern Munich - 2.44
Manchester City - 1.97
Arsenal - 1.95
Chelsea - 1.59
Liverpool - 1.33
Juventus - 1.21
Tottenham - 1.01
**Chanzo: KPMG
+++++++++++++++++++++
Kwa mujibu wa KPMG, Mwaka huu Klabu 10 zimewezwa kuvuka Thamani ya Euro Bilioni 1 huku Tottenham Hotspur na Juventus zikitinga 10 Bora kwa mara ya kwanza.
Tottenham imeing’oa Klabu ya France Paris Saint-Germain kutoka Nafasi ya 10 na kukaa wao.
Licha ya England kuwa na Klabu 6 kwenye 10 Bora, Spain ndio Nchi pekee yenye Klabu 2 zenye Thamani ya Zaidi ya Euro Bilioni 2.
MAN UNITED KUISHUPALIA REAL INAYOMTAKA DE GEA!
Mwaka 2015, Real Madrid, ambao Jumamosi wako huko Cardiff, Wales kucheza Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Juventus huku wakiwania kutetea Taji lao na kuwa Klabu ya Kwanza kufanya hivyo, walijaribu kumnunua De Gea lakini Dili ikakwama Dakika za mwisho katika Siku ya Mwisho ya Uhamisho huku pande zote zikiwa zimeafikiana Dau la Pauni Milioni 29.
De Gea, mwenye Miaka 26, alipigwa Benchi kwenye Fainali ya UEFA EUROPA LIGI hapo Mei 24 Man United wakiichapa Ajax 2-0 na kutwaa Kombe na langoni aliwekwa Kipa wa Timu ya Taifa ya Argentina Sergio Romero.
Hivi sasa, kama ilivyo kawaida ya Spain, Magazeti ya huko hushabikia mno Klabu kubwa na yale ya upande wa Real Madrid kila kukicha hawakosa kupiga ‘mdogo mdogo’ kuhusu De Gea kutua kwa Mabingwa hao wa Spain.
Lakini hivi sasa, kupita ule Mwaka 2015 ambao De Gea alikuwa kwenye Mwaka wa Mwisho wa Mkataba wake, Kipa huyo mahiri ana Mkataba unaokwisha 2019 na hivyo Man United hawana presha kubwa.
Hadi sasa, habari toka ndani ya Klabu ya Man United, zimedokeza kuwa De Gea hajaomba Uhamisho kama ilivyo kwa Wachezaji ambao wana nia hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni