UEFA EUROPA LIGI: LEO MAN UNITED KUIVAA CELTA VIGO, KUWANIA FAINALI!
MOURINHO: ‘HII NI MECHI YETU YA MSIMU!’
Nusu Fainali – Mechi za Marudiano
**Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Magoli Mechi ya Kwanza
Alhamisi Mei 11
2205 Manchester United v Celta Vigo [1-0]
2205 Olympique Lyonnais v Ajax Amsterdam [1-4]
+++++++++++++++++++++++++++++
Hilo lilitokana na ukweli kuwa Bingwa wa UEL hucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI wakati sasa Man United wanashikilia Nafasi ya 6 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, wakiwa nje ya 4 Bora huku Mechi zikibaki 3 tu na hivyo hatarini kuikosa UCL Msimu ujao.
Jana Meneja huyo wa Man United, Jose Mourinho, alisisitiza kuwa wao kuipa kipaumbele UEFA EUROPA LIGI si makosa wala kucheza tombola kwani ndio ukweli.
Hii Leo Man United wanatinga kwao Old Trafford wakiwa kifua mbele 1-0 baada ya kuifunga Celta Vigo Ugenini Wiki iliyopita.
Mourinho, akisisitiza msongo wa Ratiba, ameeleza: “Mechi 17 ndani ya Wiki 7 si mchezo. Hii [KUTILIA MKAZO UEL] si tombola ndio hali yetu! Ulikuwa uamuzi rahisi kufuatana na hali yetu!”
Mourinho amesema hatasikitika ikiwa hawatatwaa Taji la UEL na kudai: “Tutaona kama tutaweza. Tukishindwa hatujali. Hatutajutia, tumejitolea kila kitu, Wachezaji na mimi!”
Ikiwa Man United watatinga Fainali hii Leo basi upo uwezekano mkubwa wa kuivaa Ajax Amsterdam ya Netherlands ambao nao Leo wapo Ugenini kucheza na Lyon lakini wao walishinda Mechi ya Kwanza 4-1
.
DONDOO ZA MECHI YA LEO:
Man United wapo kwenye Mechi ya Leo wakiwa 1-0 mbele kwa Bao la Mchezaji wa Miaka 19 Markus Rashford, anaevaa Jezi Namba 19, kufunga Bao lake la 19 Msimu huu.
Wakati Jumapili, Celta Vigo wakipata kipigo chao cha 5 mfululizo kwa kuchapwa 3-0 na Malaga kwenye La Liga, Man United walifungwa 2-0 na Arsenal kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, Mechi ambayo walichezesha Kikosi tofauti kidogo na rekodi yao ya kutofungwa Mechi 25 za Ligi kuvunjwa.
Msimu huu, Man United wamecheza Mechi 6 za Ulaya Uwanjani kwao Old Trafford na kushinda zote.
Nini Mameneja Wamesema?
-Eduardo Berizzo, Celta Vigo:
“Nategemea Man United kushambulia ili washinde..ni mtihani mkubwa. Man United ni Timu kubwa na huishi na na presha na wanaikabili kila Siku. Inabidi tutilie mkazo tunachoweza kufanya wenyewe!”
-José Mourinho, Manchester United
“Vikombe ni muhimu kwa Klabu na ni muhimu zaidi kuwa kwenye Fainali. Ni muhimu kwa Klabu hii kupigania Kombe ambalo hawajawahi kulibeba. Tutapigana kwa nguvu. Ni safari ndefu, Mechi ya 14 Ulaya kwenye EUROPA LIGI na tunataka kushinda”
VIKOSI:
MANCHESTER UNITED: Romero; Valencia, Bailly, Blind, Darmian; Fellaini, Herrera, Pogba; Lingard, Rashford, Mkhitaryan.
NJE - Majeruhi: Shaw, Ibrahimovic, Rojo
CELTA VIGO: Sergio; Mallo, Cabral, Roncaglia, Jonny; Radoja, Tucu; Wass, Aspas, Sisto; Guidetti.
NJE - Majeruhi: Rossi, Planas
REFA: Ovidiu Alin Hategan[Romania]
UEFA EUROPA LIGI
Tarehe Muhimu:
FAINALI
24 Mei 2017: Friends Arena, Solna, Sweden
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni