tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

1 Juni 2017

HII NDIYO KLABU  DUNIANI INAYOJIENDESHA BILA MATAKWA YA MASHABIKI  WAKE
Poleni sana mashabiki wa Arsenal kwa hili.

Hakika ni neno “pole” tu ndilo linalofaa kuwapa mashabiki wa Arsenal kwani pamoja na vita waliyojaribu kupigana na kupiga kelele mtandaoni kwa muda mrefu lakini mambo yameenda tofauti na walivyotaka.
Kila mshabiki wa Arsenal alikuwa na kauli moja tu “Wenger Out” lakini sasa ni “Wenger In” kwani kocha huyo haendi popote na atabaki katika klabu hiyo kwa miaka miwili zaidi hata kama mashabiki hawapendi.
Kuna wengine walidhani labda ili kulinda heshima yake Wenger angekataa mkataba mpya na kuondoka bila kutimuliwa, lakini mzee huyo wala hajasikia na amekubali ofa ya mkataba mpya wa miaka miwili.
Taarifa zinadai siku ya Jumanne mmiliki wa klabu ya Arsenal bwana Stan Kroenke alikutana na Arsene Wenger na kukubaliana juu ya mkataba huo ambapo taarifa rasmi kutoka klabuni zilipangwa kutolewa siku ya Jumatano.
Wenger anapewa mkataba mpya baada ya Arsenal kubeba ubingwa wa FA lakini wakimaliza nje ya top four kwa mara ya kwanza toka mwaka 1996 na wamiliki wa klabu hiyo wanaamini Wenger ndio mtu pekee ambaye atawarudisha juu.

Hakuna maoni: