Klabu za Epl zajazana kumi bora ya klabu zenye thamani kibiashara Duniani.
Utafiti uliofanywa na wataalamu wa masula ya kibiashara katika soka,umegundua kwamba japokuwa klabu ya Manchester United haikuwepo katika michuano ya Champions League msimu uliopita lakini thamani ya klabu hiyo kibiashara ni kubwa kuliko timu yoyote duniani.
Thamani ya mabingwa hao wa Europa League ni £3.07bn ikiwa ni juu ya mabingwa wa Champions League ambao thamani yao kibiashara ni £2.97bn, Real Madrid nao wako juu ya Barcelona walioko nafasi ya tatu wakiwa na thamani ya £2.76bn.
Nafasi ya nne ni klabu ya Bayern Munich ambao wenyewe ni mabingwa wa soka wa nchini Ujerumani na wana thamani ya £2.44bn wakifuatiwa na Manchester City wenye thamani ya £1.97bn.
Arsenal wako nafasi ya sita wakiwa na thamani ya £1.95bn wakifuatiwa na mabingwa wapya wa soka nchini Uingereza Chelsea ambao wenyewe wana thamani ya £1.59bn.
Liverpool wenyewe wako nafasi ya nane wakiwa na thamani ya £1.33bn na Juventus wako nafasi ya tisa na thamni ya £1.21bn huku Tottenham wakimaliza 10 bora wakiwa na
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni