Wakati dunia ikikumbuka kustaafu kwake, haya ni mambo 15 ya kufahamu kuhusu Pele
Ni uzao wa mshambuliaji wa kikosi cha Brazil cha miaka ya 1930’s – João Ramos do Nascimento na mwanamama Celeste Arantes.
1.Ni baba wa watoto sita, Sandra Machado, Kelly Cristina, Flávia Kurtz, Edinho, Joshua na Celeste.
2.Inasadikika ndio mchezaji bora wa wakati wote wa soka, akiwa na rekodi ya kucheza jumla ya mechi 1281 na kufunga magoli 1363.
3.Ameshinda ubingwa wa dunia na Brazil mara 3 na Copa America mara 1. •Mfungaji bora wa muda wote wa Brazil (Magoli 95)
4.Ana rekodi ya dunia ya kufunga hat tricks 92
•Mfungaji mdogo zaidi katika michuano ya kombe la dunia, mfungaji – miaka 17 na siku 239 (Brazil v Wales 1958)
5.Mfungaji wa hat trick mdogo zaidi katika World Cup – miaka 17 na siku 244 (Brazil v France 1958)
6.Mfungaji mdogo zaidi katika mchezo wa fainali ya Kombe la dunia na mshindi wa taji hilo – miaka 17 na siku 249.
7.Lakini pia kama hufahamu tu ni kwamba Pele ndio mchezaji aliyeipa umaarufu style ya aina ya Bycle Kick baada ya kufunga bao kwa style hiyo.
8.Waldemar De Brito ni mchezaji wa zamani wa Santos na ndiye aliyempeleka Pele kucheza soka na siku aliyompeleka alimuambia kocha kwamba “huyu kijana atakuwa bora duniani”
9.Kwa kutambua mchango wa Pele, mwaka 1995 serikali ya Brazil ilimpa uwaziri wa michezo, alidumu katika cheo hicho hadi 1998.
10.Katika klabu ya Santos kila tarehe 19 November wanasheherekea Pele Day ambapo ndiyo siku ambayo Pele alifunga bao lake la 1000.
11.Baada ya Pele kustaafu, balozi wa Marekani nchini Brazil alinukuliwa akisema “kwa miaka 22 aliyocheza soka ameeneza amani na upendo kuliko ubalozi wowote ule duniani”
12.Muandishi mmoja wa vitabu Uingereza aliulizwa kuhusu tofauti ya Pele na wachezaji wengine akiwemo Di Stefanio na alijibu “Di Stefanio amezaliwa lakini Pele ametengenezewa mbinguni”
13.Jina la Pele ilikuwa nickname yake shuleni lakini familia yake ilimtambua kwa nickname ya Dico.
14.Pamoja na umahiri wake wote lakini Pele hajawahi kuvunja rekodi ya baba yake, baba mzazi wa Pele ameshawahi kufunga mabao 5 ya vichwa katika mchezo mmoja huku Pele magoli mengi ya vichwa katika mechi 1 ni manne.
15.Wazazi wake Dondinho na Celeste walimpa jina la Edson Arantes do Nascimento – ulimwengu wa soka unamtumbua kama #PELE – siku kama ya leo, Oktoba mwaka 1977 Pele alistaafu kucheza soka akiwa na klabu ya Cosmos ya nchini Marekani.
Pique azidi kuchafua hali ya hewa Hispania, bifu lake na Ramos lafika pabaya
Kwa muda mrefu Gerrard Pique amekuwa akiwarushia rushia vijembe Real Madrid, Pique amekuwa akifanya mashambulizi dhidi ya Real Madrid kwa njia ya maandishi na mahojiank hali ambayo humkera captain wa Madrid Sergio Ramos.
Hilo likapita, lakini sasa Pique amekuja na jipya ambalo ni kubwa zaidi. Pique amekuwa mstari wa mbele kuishambulia serikali ya Hispania kwa kitendo chao cha kuzuia kura za maoni za wananchibwa Catalunya kudai uhuru wao.
Pique ambaye ni raia wa Catalunya amesema wazi wazi kutokubaliana na askari wa Hispania jambo ambalo Ramos amelipinga, Ramos anaona sio jambo jema kwa mchezaji wa Hispania kujihusisha sana na masuala hayo.
Ramos anaona anachofanya Pique kinaweza kuleta mpasuko katika timu ya taifa na kuwagawa Wacatalunya na Wahispania wakati wakiwa timu ya taifa wote wanakuwa kitu kimoja tu.
Wakati hayo yabRamos na Pique yakiendelea tayari mpasuko katika timu ya taifa umeanza kuonekana baada ya hapo jana kuonekana mabango ya kumtukana Gerrad Pique wakati wa mazoezi ya timu ya taifa.
Gazeti moja kubwa nchini Hispania limesema Gerrard Pique ambaye pia ni beki pacha wa Ramos katika timu ya taifa anaweza kulazimishwa kustaafu kuichezea timu ya taifa kutokana na mpasuko huo.
Moja kati ya mabango ambayo yalibebwa wakati wa mazoezi ya Hispania liliandikwa “Pique hatutaki ujitoe timu ya taifa tunataka ufukuzwe” na lingine likiandikwa “mama yangu alisema kama unataka kuwa huru basi ondoka nyumbani”
Timu ya taifa ya Hispania inatarajiwa kuwa na michezo miwili ndani ya siku 3 kuanzia tarehe 6 watakapokipiga na Albania huku siku 3 baadae watakwenda hadi Israel kukipiga na timu ya taifa ya Israel.
Nukuu 5 za siku, Cr7 aeleza sababu ya kuondoka Manchester United
Kona ya nukuu 5 za siku itakuwa inakuletea walichosema wachezaji wakubwa, makocha na wadau mbali mbali wa soka barana Ulaya na pande za kimataifa.
“Old Tarford siwezi kupasau ndio sehemu ilinifanya kuwa karibu na wachezajibwakubwa duniani lakini nilihitaji kuonesha nini naweza kufanya katika timu nyingine ndio maana nilikuja Madrid” Cristiano Ronaldo.
Mchezaji wa soka wa zamani wa Liverpool Steven Gerrad amesema haya kuhusu Harry Kane “ana kila kitu ambacho mshambuliaji anapaswa kuwa nacho, nafarijika kwa kuwa ni Muingereza lakini nitafurahi zaidi akiwa Liverpool”
Marcus Rashford naye kuhusu kiwango chake anasema “mara zote nikiwa uwanjani huwa najitahidi sana kucheza katika kiwango cha Lukaku na Harry Kane,hao ndio wanakuwa katika mawazo yangu”
Arjen Robben naye amefunguka yake kuhusu tetesi za yeye kufurahia kufukuzwa kwa Carlo Ancelotti “hizo wanazosema ni nukuu zangu ni ujinga, mimi huwa sipendi mambo hayo na siwezi kutokuwa vizuri na Carlo”
“Kama siku moja akafunga safari kuja Uingereza kunisalimia baasi hapo hapo nitaanza kumshawishi ahamie Arsenal” hayo ni manenl ya mshambulia Alexandre Lacazette kuhusu nyota wa Athletico Madrid Antoine Griezman.
Arsene Wenger apatwa na hofu kuhusu Barcelona kuhamia Epl
Masuala ya kisiasa yanayoendelea nchini Hispania tayari yameleta habari nyingi za kisoka, lakini kubwa ni uwezekano wa vilabu vya Catalunya kuhamia katika ligi zingine ikiwemo Epl.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anaonekana kutofurahia habari za Barcelona kuhamia katika ligi kuu ya Uingereza huku akihoji Barcelona watahamiaje wakati kuna vilabu vya Scotland havijahamia hadi leo.
Wenger amesema haitakuwa sahihi kwa FA kuruhusu jambo hilo kutokea huku wakivikatalia vilabu vya nchi jirani ya Scotland kuhamia katika ligi hiyo.
Sii hivyo tu lakini mzee Wenger ameonya kuhusu mbio za ubingwa wa Epl kwamba zinaweza kuwa ngumu mno kama miamba hiyo ya La Liga itapewa ruhusa kujiunga na ligi kuu Uingereza.
Wiki iliyopita waziri mwenye dhamana ya michezo nchini Hispania alisema vilabu vya Catalunya vinaweza kuhamia katika ligi za jirani endapo Catalunya watapata uhuru wao.
AC Milan na Inter Milan hawana mpango wa kutengana
Vilabu viwili vikongwe katika ligi ya mpira ya nchini Italia Ac Milan na Inter Milan wameungana katika suala la kuboresha kiwanja chao cha nyumbani cha San Siro ili kuonekana bora zaidi.
Wawakilishi wa vilabu hivyo walikutana na meya wa jiji la Milan Giussepe Sala ili kuongea juu ya utengenezaji huo mpya wa uwanja wao ambao unaingiza mashabiki 80,000.
Vilabu vyote viwili viko tayari kuchangia kifedha utengenezaji huo ambapo wanaona San Siro imekaa kizamani na kujaribu kuufanya kuonekana wa kisasa zaidi kwa kufanya marekebisho makubwa.
Makubaliano haya kati ya Ac Millan na Inter Milan yanafuta tetesi ambazo zilizagaa kwamba moja kati ya vilabu hivi viwili watahama uwanja huu siku za usoni, kwani hii inaonesha jinsi gani wote hawana mpango wa kuondoka San Siro.
Giussepe Sala amesifu mpango huo wa Ac Milan na Inter Milan na akasisitiza kwamba sio faida tu kwa vilabu hivyo viwili lakini uwepo wa uwanja bora utaongeza thamani ya jiji la Milan.
Raisi Vladmir Putin aingilia kati maandalizi ya kombe la dunia
Fainali za kombe la dunia mwakani zinapigwa nchini Urusi, mataifa mbali mbali hata wale ambao timu zao hazitashiriki kombe hilo watakuwepo nchinj Urusi kutazama michuano hiyo mikubwa zaidi duniani.
Kwa sasa imebaki miezi kadhaa tu twende Urusi lakini unaambiwa nchini humo bado sana yani ndio kwanzaaa wako nyuma sana katika maandalizi utafikiri mashindano hayo ni 2020.
Hali hii ya kusua sua kwa maandalizi imemkera raisi wa Urusi Vladmir Putin na kusema kwamba hawezi kukubali taifa lake kuonekana nyuma kutokana na uzembe wa watu wachache wa soka.
Putin amesema anaingiwa na hofu kwamba fainali hizo zitafika huku maandalizi yakiwa hayajakamilika jambo ambalo linaweza kuichafua nchi ya Urusi na kutoa sifa mbaya kwake.
Pamoja na kuandaa kombe la Shirikisho Fifa mwezi June lakini Urusi inaonekana bado viwanja vingi havijakamilika na bado sana hawajaweka mikakati kuhusu kukabiliana na wimbi la wageni watakaokwenda Urusi.
Michuano ya kombe la dunia inataraji kupigwa kuanzia June mwakani hadi July mwakani na tayari Urusi wameandaa kadi maalum kwa ajili ya usalama wa mashabiki watakaokuwa hapo.
Arsenal yakaribia kumilikiwa na mtu mmoja, wazee wapinga
Kwa muda sasa kumekuwa na majaribio ya chinichini kati ya wamiliki wakubwa wa hisa za klabu ya Arsenal kuhusu kujaribu kuinunua klabu hiyo, Alisher Usmananov na mmiliki mkuu wa hisa za klabu Stan Kroenke wamekuwa wakitunishiana misuli.
Mwezi wa tano mwaka huu Usmananov raia wa Urusi alifanya jaribio la kuimiliki klabu ya Arsenal kwa kujaribu kumiliki hisa zote za klabu hiyo lakini jambo hilo halikuwezekana kutokana na kuwekea ngumu na Kroenke.
Sasa Stan Kroenke ambaye anamiliki 67% ya hisa za klabu ya Arsenal ameamua kutangaza ofa ya £528m ambapo kila hisa atainunua kwa £28,000 kiasi amabacho kinasemekana kinaweza kumvutia Usmananov.
Usmananov anamiliki 30% za klabu hiyo, lakini japokuwa Usmananov na Kroenke wamekuwa wamiliki wakubwa wa hisa katika klabu hiyo kwa muongo mmoja sasa lakini matajiri hao wawili hawana uelewano mzuri katika kazi.
Kama Kroenke atafanikiwa kununua hisa za Usmananov baasi atamiliki 97% ya hisa za Arsenal na huku 3% zinazobaki zikibaki kwa wamiliki wadogo wa Arsenal ambao wengi ni wazee wa kitambo wa klabu hiyo.
Umiliki wa 97% kwa Kroenke utakuwa umemuweka kwenye nafasi nzuri kujaribu kushawishi kuchukua hisa 3% zilizobakia na hali hii moja kwa moja itamfanya kuimiliki Arsenal na vitu vyake vyote.
Lakini wakati Kroenke anajaribu kununua hisa za Usmananov, wamiliki wadogo wa hisa za Arsenal ambao wengi wapo Arsenal kwa ajili ya mapenzi yao na klabu hiyo na sio faida ya kifedha kama ilivyo kwa Usmananov na Karoenke hawakubaliani na jaribio hilo.
Msemaji wao ameonesha hofu ya klabu kupelekwa itakavyo na mtu mmoja huku akihoji kama Karoenke anaona anaweza jukumu hilo mbona timu haifanyi vizuri? Lakini pamoja na yote hayo ni wazi Usmananov kuna asilimia kubwa atauza hisa zake.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni