AC MILAN YAAMUA KUJIIMARISHA, YAANZA NA BACCA, YATENGA EURO MILIONI 30
Klabu ya AC Milan imefikia makubaliano ya kumsajili
mshambuliaji Carlos Bacca raia wa Colombia.
Milan imekubali kutoa eur milioni 30 kumnasa Bacca aliyetoa
mchango mkubwa na kuisaidia Sevilla kutwaa ubingwa wa Europa.
Kwa mujibu wa gazeti la La Gazzetta dello Sport la nchini
Italia, kwamba mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 ni chaguo la kwanza la Milan
ambayo imejipanga kujiboresha.
Milan imekuwa na msimu mbaya katika msimu uliopita na sasa imepania kufanya usajili kamambe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni