COPA AMERICA: BRAZIL NJE, PARAGUAY YASHINDA
Katika 90 za kawaida, Mzoefu Robinho aliipa Bao Brazil Dakika ya 15 alipounganisha Krosi safi ya Dani Alves.
Bao hilo lilidumu hadi Haftaimu.
Paraguay walisawazisha kwa Penati ya Derlis González katika Dakika ya 72 baada ya Silva kuunawa Mpira.
Hadi Dakika 90 kwisha Bao zilikuwa 1-1 na ndipo ikaja Tombola ya Mikwaju ya Penati Tano Tano.
Timu zote zilifunga Penati zao za kwanza kwa Brazil kupitia
Fernandinho na Paraguay kupitia Martinez lakini Brazil wakakosa ya Pili
aliyopiga Ribeiro na Caceres kuifungia Praguay na kuongoza 2-1.
Brazil walisawazisha kwa Penati ya Miranda na Paraguay kwenda 3-2
kwa Penati ya Bobadilla huku Douglas Costa akiikosesha Brazil Penati ya 4
na kuwafanya wawe nyuma 3-2 lakini Santa Cruz, ambae alitakiwa afunge
tu na kuipa ushindi Paraguay, nae alikosa.
Penalti ya mwisho ya Brazil ilifungwa na Coutinho lakini Paraguay
wakashinda Mechi hii kwa Penati yao ya 5 na ya mwisho iliyopigwa na yule
yule aliewasazishia kwa Penati ndani ya Dakika 90, Derlis González.
Matokeo haya yanaifanya Paraguay, kwa mara ya pili mfululizo,
kuitoa Brazil kwenye Mashindano haya, kwenye hatua hii hii, kwa Mikwaju
ya Penati kwani Mwaka 2011 huko Argentina waliwabwaga Brazil kwa Penati
2-0 baada ya Brazil kukosa Penati zao zote 4.
Paraguay sasa wapo Nusu Fainali na watacheza na Argentina hapo
Jumanne wakati Jumatatu ni Nusu Fainali nyingine kati ya Wenyeji Chile
na Peru.
VIKOSI:
Brazil ( Mfumo 4-2-3-1): Jefferson; Alves, Silva, Miranda, Luis; Fernandinho, Elias; Willian, Coutinho, Robinho; Firmino.
Paraguay ( Mfumo 4-4-2): Villar; Aguilar, Da Silva, Bruno Valdez,
Piris; Gonzalez, Caceres, Aranda, Benitez; Santa Cruz, Nelson Valdez.
REFA: Andrés Cunha (Uruguay)
COPA AMERICA
RATIBA/MATOKEO:
ROBO FAINALI
Jumatano Juni 24
Chile 1 Uruguay 0
Alhamisi Juni 25
Bolivia 1 Peru 3
Ijumaa Juni 26
Argentina 0 Colombia 0 (Penati-Argentina washindi 5-4)
Jumamosi Juni 27
Brazil 1 Paraguay 1 ( Penati-Paraguay washindi 4-3 )
NUSU FAINALI
Jumatatu Juni 29
Chile v Peru (Saa 8 na Nusu Usiku)
Jumanne Juni 30
Argentina v Paraguay (Saa 8 na Nusu Usiku)
MSHINDI WA 3
Ijumaa Julai 3
(Saa 8 na Nusu Usiku)
FAINALI
Jumamosi Julai 4
(Saa 5 Usiku)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni