EURO U-21: PORTUGAL YAIBONDA GERMANY 5-0, FAINALI KUIVAA SWEDEN!
Portugal wametinga Fainali kwa kuibonda Germany 5-0 na Sweden wamewachapa jirani zao Denmark 4-1.
Portugal na Sweden walikuwa Kundi moja kwenye Mashindano haya na kutoka Sare 1-1.
Bao za Portugal, chini ya Kocha Rui Jorge, katika Mechi yao na
Germany zilifungwa na Bernardo Silva, Ricardo, Ivan Cavaleiro katika
Kipindi cha Kwanza na João Mário na Ricardo Horta kufunga Kipindi cha
Pili.
Baada ya kuwa nyuma 5-0, Germany, walibaki Mtu 10 baada ya Leonardo Bittencourt kupewa Kadi Nyekundu.
Nao Sweden waliongoza 2-0 hadi Haftaimu kwa Bao za Penati ya John
Guidetti na Simon Tibbling na Kipindi cha Pili kuanza kwa Denmark kupata
Bao lao moja kupitia Uffe Bech lakini Sweden waliongeza 2 nyingine
kupitia Robin Quaison na Oscar Hiljemark na kushinda 4-1.
Fainali ya U-21 itachezwa Jumanne Juni 30 na kuzikutanisha Swden na
Portugal ambayo mara ya mwisho kucheza Fainali kama hii ni Mwaka 1994
wakiongozwa na Chipukizi Luís Figo na Rui Costa ambao waliibuka kuwa Masupastaa wa Dunia.
MAKUNDI
KUNDI A
**Kila Timu imecheza Mechi 3
1 Denmark Pointi 6
2 Germany 5
3 Czech Rep 4
4 Serbia 1
KUNDI B
**Kila Timu imecheza Mechi 3
1 Portugal Pointi 5
2 Sweden 4
3 Italy 4
4 England 3
****Timu 2 za juu za kila Kundi zitasonga Robo Fainali
RATIBA/MATOKEO:
**Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumapili Juni 21
Sweden 0 England 1
Italy 0 Portugal 0
Jumanne Juni 23
Czech Republic 1 Germany 1
Denmark 2 Serbia 0
Jumatano Juni 24
England 1 Italy 3
Portugal 1 Sweden 1
NUSU FAINALI
Jumamosi Juni 27
Demark 1 Sweden 4
Germany 5 Portugal 0
FAINALI
Jumanne Juni 30
Portugal v Sweden
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni