tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

19 Juni 2015

COPA AMERICA: CLAUDIO PIZARRO ALIFUMUA KUNDI C, TIMU ZOTE 4 POINTI 3, MECHI BADO 1!!

COPA-AMERICA15Bao la Dakika ya 72 la Claudio Pizarro limeipa ushindi Peru wa Bao 1-0 walipocheza na Venezuela katika Mechi ya Kundi C la Copa America huko Estadio Elias Figueroa Brander Mjini Valparaiso Nchini Chile na kulifumua Kundi lao kuwa wazi.
Sasa kwenye Kundi C kila Timu ina Pointi 3 na imebakisha Mechi moja tu.
Kwenye Mechi hii, Peru, ambao ilikuwa lazima washinde baada ya kufungwa Mechi yao ya kwanza na Brazil, waliikuta Venezuela imesimama kidete licha ya kucheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 29 baada ya Beki wao Fernando Amorebieta kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa kumtimba Paolo Guerrero.
Hata hivyo, Mkongwe Claudio Pizarro mwenye Miaka 36 alietokea Benchi na ambae sasa hana Timu baada kumaliza Mkataba wake na Bayern Munich, aliweka hai matumaini ya Peru baada kufumua Shuti lililomshinda Kipa Alain Baroja.
++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
KUNDI A
**Kila Timu imecheza Mechi 2
1 Chile Pointi 4
2 Bolivia 4
3 Mexico 2
4 Ecuador 0
KUNDI B
**Kila Timu imecheza Mechi 2
1 Argentina Pointi 4
2 Paraguay 4
3 Uruguay 3
4 Jamaica 0
KUNDI C
**Kila Timu imecheza Mechi 2 
1 Peru Pointi 3 
2 Brazil 3
3 Colombia 3
4 Venezuela 3 
**Timu 2 za Juu kila Kundi na Timu za 3 mbili Bora zitasonga Robo Fainali
++++++++++++++++++++++
Leo zipo Mechi mbili za mwisho za Kundi A ambpao Wenyeji Chile watamaliza na Bolivia na Ecuador kucheza na Mexico.
COPA AMERICA 
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Alhamisi Juni 11
KUNDI A Chile 2 Ecuador 0
Ijumaa Juni 12
KUNDI A Mexico 0 Bolivia 0
Jumamosi Juni 13
KUNDI B Uruguay 1 Jamaica 0
KUNDI B Argentina 2 Paraguay 2
Jumapili Juni 14
KUNDI C Colombia 0 Venezuela 1
KUNDI C Brazil 2 Peru 1
Jumatatu Juni 15
KUNDI A Ecuador 2 Bolivia 3
KUNDI A Chile 3 Mexico 3
Jumanne Juni 16
KUNDI B Paraguay 1 Jamaica 0
KUNDI B Argentina 1 Uruguay 0
Jumatano Juni 17
KUNDI C Brazil 0 Colombia 1
Alhamisi Juni 18
KUNDI C Peru 1 Venezuela 0
Ijumaa Juni 19
KUNDI A Mexico v Ecuador (Saa 6 Usiku)
KUNDI A Chile v Bolivia (Saa 8 na Nusu Usiku)
Jumamosi Juni 20
KUNDI B Uruguay v Paraguay (Saa 4 Usiku)
KUNDI B Argentina v Jamaica (Saa 6 na Nusu Usiku)
Jumapili Juni 21
KUNDI C Colombia v Peru (Saa 4 Usiku)
KUNDI C Brazil v Venezuela (Saa 6 na Nusu Usiku)
ROBO FAINALI
Jumatano Juni 24
A1 v B3/C3 (Saa 8 na Nusu Usiku)
Alhamisi Juni 25
A2 v C2 (Saa 8 na Nusu Usiku)
Ijumaa Juni 26
B1 v A3/C3 (Saa 8 na Nusu Usiku)
Jumamosi Juni 27
C1 v B2 (Saa 6 na Nusu Usiku)
NUSU FAINALI
Jumatatu Juni 29
RF1 v RF2 (Saa 8 na Nusu Usiku)
Jumanne Juni 30
RF3 v RF4 (Saa 8 na Nusu Usiku)
MSHINDI WA 3
Ijumaa Julai 3
(Saa 8 na Nusu Usiku)
FAINALI
Jumamosi Julai 4
(Saa 5 Usiku)
 

Hakuna maoni: