OFFICIAL: LIVERPOOL YAIZIDI KETE MAN UNITED KWA KUMSAJILI STRAIKA HUYU….
Liverpool imethibitisha rasmi
kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Roberto Firmino kutoka klabu ya
Hoffenheim kwa dau la paundi milioni 29.
Firmino mwenye miaka 23
amesaini mkataba wa miaka mitano ambao atakuwa akilipwa mshahara wa
paundi laki moja kwa wiki na anaungana na Wabrazil wenzake
Anfield, Philippe Coutinho na Lucas Leiva
Hata hivyo, Firmino haendi
kuchukua vipimo vya afya mpaka Brazil itakapotoka kwenye michuano ya
Copa America inayoendelea nchini Chile.
Mshambuliaji huyo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Majogoo kwa dau kubwa zaidi kihistoria kwani Andy Carroll, alisajiliwa kwa paundi milioni 35 mwezi Januari 2011
Mkurugenzi mkuu wa Liverpool,
Ian Ayre alisafiri mpaka Chile usiku wa kuamkia leo na kukamilisha
usajili wa Firmino ambaye alikuwa anawindwa pia na Manchester United.
Hii ndio Tweet ya Liverpoool asubuhi hii:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni