tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

22 Juni 2015

NANI ATACHEZA NA NANI ROBO FAINALI YA COPA AMERICA…RATIBA HII HAPA.

Copa-America-2015Michuano ya kombe la mataifa ya America Kusini maarufu kama Copa America imeingia kwenye hatua ya robo fainali baada ya michezo ya Kundi C kumalizika usiku wa kuamkia leo.
Robo fainali ya kwanza itawakutanisha wenyeji wa michuano hiyo timu ya Chile itakuwa ikikipiga dhidi ya Uruguay siku ya Jumatano, Chile watahitaji ushindi kwa nguvu zote kwasababu wao ndio wenyeji wa michuano hivyo watataka kuhakikisha wanafika mbali kwenye mashindano hayo wakiwa kwenye ardhi ya nyumbani wakiongozwa na nyota wao wa Arsenal Alexis Sanchez na kiungo wa Juventus Aturo Vidal.
Lakini Cavani, Godin na nyota wengine wengi wa Uruguay watakuwa tayari kuwakabili Chile kwenye mchezo huo wa robo fainali ya kwanza.
Bolivia wao watakipiga dhidi ya Peru kwenye robo fainali ya pili itayochezwa siku ya Alhamisi. Bolivia imewashangaza wengi kwa kutinga kwake hatua ya robo fainali kwasababu wengi walikuwa wakiibeza na kutoipa nafasi kwenye michuano ya mwaka huu. Lakini mshambuliaji wa Bayern Munich Claudio Pizarro anatarajiwa kukiongoza kikosi cha Peru kuikabili Bolivia.
Mchezo mwingine utakaovuta hisia za watu wengi ni ule ambao Argentina itakapochuana na Colombia kwenye robo fainali ngumu na ya kukata na shoka itakayopigwa siku ya Ijumaa.
Nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Messi atakuwa akiwaongoza nyota wengine kama Di Maria, Aguero, Tevez na wengine wengi kutafuta ushindi mbele ya Colombia ambayo inaongozwa na nyota wa Madrid James Rodriguez na wenzake kama Cuadrado na Falcao.
Brazil watakipiga dhidi ya Paraguay kwenye robo fainali ya mwisho itakayochezwa Jumamosi. Brazil bado itaendelea kumkosa Neymar na itakuwa ikitupa karata yake ya pili kujaribu kutafuta ushindi bila nyota huyo aliyefungiwa mechi nne.
Ratiba kamili ya robo fainali hii hapa;
Chile v Uruguay – Jumatano
Bolivia v Peru – Alhamisi 
Argentina v Colombia – Ijumaa
Brazil v Paraguay – Jumamosi

Hakuna maoni: