LIVERPOOL WAPIGWA KANZU NA AC MILAN……
Mshambuliaji wa Sevilla, Carlos Bacca amethibitisha kufikia makubaliano binafsi na miamba ya kandanda Italia, AC Milan.
Wakala wa Bacca, 28, Sergio
Barila, ameliambia gazeti la Marca mwishoni mwa Juma lililopita kwamba
Straika huyo amekubaliana na Milan na yuko tayari kujiunga na timu hiyo.
Bacca mwenyewe amewathibitishia waandishi wa habari nchini Colombia kuwa tayari wamekubaliana na Milan.
“Inahitaji kuthibitishwa,
lakini kwa kujiamini kabisa alichosema wakala wangu ni sahihi. Tumefikia
makubaliano na Milani ambayo ina asilimia 100 za kunisajili”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni