Juventus
wamemsajili mshambuliaji Mario Mandzukic kutoka Atletico Madrid kwa
pauni milioni 13.6. Mshambuliaji huyo raia wa Crosia alijiunga na
Atletico mwaka jana akitokea Bayern Munich na alifanikiwa kupachika
mabao 20 katika mechi 43 alizocheza. Mandzukic amesaini mkataba wa miaka
minne.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni