“HATA LIONEL MESSI ANGEPATA WAKATI MGUMU KUVAA VIATU VYAKE”
James Milner amesisitiza kwamba
hakuna mchezaji yeyote katika sayari hii anayeweza kurithi viatu vya
nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard katika dimba la Anfield.
Milner, 29, ambaye amejiunga na
Liverpool majira haya ya kiangazi akiwa mchezaji huru amesema hata
Mwanasoka bora mara nne wa Dunia, Lionel Messi hawezi kurithi mikoba ya
Gerrard.
“Sidhani kama kuna mtu
yeyote kwenye sayari hii ambaye anaweza kuvaa viatu vya Gerrard Anfield
na kufikia mambo yote aliyoyafanya kwa miaka yote aliyodumu. Sisi kama
timu tunahitaji kurithi jitihada zake”. Amewaambia ABC.
“Kwa yale aliyofanya Stevie,
hata Messi (Lionel) angepata wakati mgumu kuvaa viatu vyake”. Ameongeza
Milner ambaye alicheza pamoja na Gerrard wakiitumikia timu ya Taifa ya
England.
“Yale aliyofanya ndani na
nje ya uwanjani, kama mchezaji, kama nahodha wa timu, kama mtu wa
kawaida, hakika yanashangaza. Ni ngumu kurithi, lakini nina uhakika kama
timu tunaweza”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni