MANENO 33 YA ARSENE WENGER AKIZUNGUMZIA UBINGWA WA PREMIER LEAGUE
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger sasa anaamini kwamba kikosi chake kipo tayari kushinda taji la ligi kuu soka England msimu ujao.
Bosi huyo wa Gunners anajiamini
kwamba timu yake itawazuia Chelsea kutetea ubingwa wao, huku akikanusha
kuwa Arsenal ni dhaifu mbele ya The Blues.
Arsenal haijawahi kushinda
kombe tangu 2004, mwaka ambao Jose Mourinho aliwasili mjini London,
lakini Wenger ambaye hajawahi kumfunga Mourinho amewaambia Independent:
“Tutashinda ubingwa msimu
ujao? huwezi kujipa uhakika katika michuano ya ligi kuu. Nataka kusema
kwamba, tutapambana kuwania ubingwa. Nikiwa kocha lazima niisaidie timu,
lakini mwisho wa siku najua mwishoni mwa msimu nitakuwa wapi”.
Kuanzia Agosti 8 mwaka huu,
Arsenal wataungana na Manchester City, Manchester United kuwania ubingwa
ambao unashikilia na Chelsea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni