WENGER AICHOKONOA MAN UNITED-'IMETUPA UTAMADUNI WAKE KUSAKA UTUKUFU!'
Katika kipindi hiki cha Dirisha la Uhamisho, Man United imetumia
karibu Milioni 80 kuwanunua Wachezaji Wanne ambao ni Memphis Depay,
Matteo Darmian, Bastian Schweinsteiger na Morgan Schneiderlin wakati
Arsenal imenunua Mchezaji mmoja tu, tena Mkongwe, Kipa Petr Cech, kutoka
Chelsea kwa Pauni Milioni 10.
Wenger, ambae husifika kwa ubahili katika kununua Wachezaji,
anahisi kutanua Misuli ya Fedha kwa Man United kunaathiri kukuza vipaji
vya Wachezaji Chipukizi na pia anaamini hima ya Meneja wao Louis van
Gaal kununua Wachezaji ni dalili Klabu hiyo imepoteza uvumulivu.
Wenger ameeleza: "Sisi tutaendeleza kuchanganya uwezo wetu Kifedha
na imani yetu katika Falsafa na Sera ya kuwapa nafasi Wachezaji
Chipukizi na kukuza Wachezaji toka ndani ya Klabu kama Utamaduni wetu
ulivyo. Kama baada ya hapo tutashindania kununua Wachezaji sawa lakini
huo hautakuwa msingi wa Sera yetu."
Wenger amefafanua: "Klabu karibu zote zilizokuwa na mafanikio
zilifanya hivyo. Zichukulie Barcelona na Man United, ambao walikuwa na
kizazi kilichokuzwa toka ndani ya Klabu. Hilo ndio utamaduni wetu na ni
muhimu kubakiza hivyo. Hilo liliwapa Man United mafanikio na kutengeneza
Fedha nyingi lakini Leo hawana uvumilivu kuendeleza hilo hilo. Wana
uwezo Kifedha kufuata Sera nyingine. Na sasa hawana kizazi cha Wachezaji
kama Paul Scholes, Ryan Giggs na David Beckham ndani ya Klabu yao."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni