MANCHESTER UNITED, PSG SASA WAZUNGUMZA LUGHA MOJA…
Manchester United wamekubali
ofa ya Euro milioni 65 kumuuza Angel Di Maria katika klabu ya Paris
Saint-Germain (PSG), hii ni kwa mujibu wa France Football.
Imeripotiwa kwamba siku chache
zilizopita Mkurugenzi mkuu wa Man United, Ed Woodward alikuwa na
mazungumzo na Mkurugenzi msaidizi wa michezo wa PSG, Olivier Letang
ambapo wamefikia makubaliano ya ada ya uhamisho ya winga huyo wa zamani
wa Real Madrid ambaye anaondoka Old Trafford baada ya kudumu kwa mwaka
mmoja tu katika soka la England.
Inafahamika kwamba PSG wanataka
kukamilisha dili hilo kabla ya wikiendi ili Muargentina huyo
aliyesajiliwa mwaka jana na Man united kwa paundi milioni 59.7 ajiunge
na wachezaji wenzake waliopo katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya
nchini Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni