SERGIO RAMOS KUBAKI REAL KWA ASILIMIA
Ipo minong'ono kuwa Man United wapo tayari kubadilisha na Real kwa
kuwapa Kipa wao David de Gea, anaesemekana kutaka kuhamia Real, na wao
kumchukua Sergio Ramos anaedaiwa kutokuwa na furaha na Real.
Hadi sasa De Gea, ambae Mkataba wake na Man United unakwisha Mwakani, amekataa kusaini Mkataba mwingine mpya.
Akiongea kabla ya Mechi yao Ijumaa na Man City huko Australia,
Benitez amesema: "Ninamuheshimu sana Meneja wao Louis van Gaal lakini
Ramos atabaki hapa. Ni Mchezaji wetu na Kepteni wetu. Kwangu mimi, nina
hakika atabaki kwa Asilimia 100."
Aliongeza: "Nasisitiza ni wazi kwangu na Klabu, Sergio atakuwa hapa. Soka ni Dunia ya kushangaza lakini Ramos atabaki!"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni