UEFA EUROPA LIGI: WEST HAM YAFUNGWA, YASONGA KWA MATUTA!
West Ham walitinga kwenye Mechi hii wakiwa Washindi wa 1-0 katika
Mechi ya kwanza iliyochezwa kwao Wiki iliyopita huko Upton Park lakini
Jana wakajikuta wakifungwa Bao katika Dakika ya 14 na Straika Fabrizio
Miccoli na kisha kujikuta wakiwa Mtu 10 katika Dakika ya 45 Defenda wao
James Tomkins alipopewa Kadi Nyekundu.
Gemu hii ilikwenda hadi Dakika 90 ikiwa 1-0, na hivyo Timu hizi
kufungana 1-1, na kuongezewa Dakika za Nyongeza 30 lakini, licha ya
Birkirkara FC nao kubaki Mtu 10 katika muda huo baada ya Mauricio
Mazzetti kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu, Mechi iliisha 1-0 hadi Dakika
120 zinamalizika.
Kwenye Mikwaju ya Penati, West Ham walifunga Penati zao zote 5 na
kushinda 5-3 na sasa wataivaa Klabu ya Romania, Astra, katika Raundi ya 3
ya Mtoano.
Mechi za Raundi ya Tatu ya Mtoano zitachezwa Julai 30 na Agosti 6
na Washindi wake watasonga Raundi ya Mchujo ambayo Washindi wake
wataingia hatua ya Makundi.
Baadhi ya Klabu maarufu huko Ulaya ambazo zitaanzia Raundi ya 3 ni
pamoja na Borussia Dortmund, Athletic Bilbao, Sampdoria, Bordeaux na
Southampton.
Klabu hizo maarufu ni miongoni mwa Klabu 25 ambazo zimeingizwa moja
kwa moja kuanzia Raundi hii ya 3 na zitajumuishwa na Washindi 33 kutoka
Raundi ya Pili ya Mtoano.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
EUROPA LIGI
Hatua za kutinga Mechi za Makundi:
-Raundi ya Pili ya Mtoano: Mechi Julai 16 na 23
-Raundi ya Tatu ya Mtoano: Mechi Julai 30 na Agosti 6
-Raundi ya Mchujo: Mechi Agosti 20 na 27
-Makundi: Mechi za kwanza Septemba 17
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni