tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

16 Septemba 2015

REKODI ZA UEFA AMBAZO MESSI NA RONALDO BADO HAWAJAZIFIKIA HADI SASA

‘Striker life is in the goal scores’ Ni usemi maarufu sana katika tasnia ya soka ukiwa na maana ya moja kwa moja kwamba maisha ya mshambuliaji yapo katika ufungaji. Mifano tunayo juu ya washambuliaji kibao ambao wamegeuka butu na kudharauliwa. Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ni washambuliaji ambao bado wanaheshimika sana duniani kutokana na uwezo wao mkubwa uwanjani. Rekodi nyingi sana zinashikiliwa na hawa jamaa katika michuano tofauti ikiwemo ile ya UEFA Champions League. Leo hii nimekuwekea rekodi ambazo hazijafikiwa na wachezaji hawa katika michuano ya UEFA Champions League, karibu sana.
WASTANI MZURI WA KUFUNGA MAGOLI
Gerd Muller wa Bayern
Munich ndiye mmiliki wa rekodi hii kwani jamaa ana wastani wa 0.97 katika mechi zote. Pia Radamel Falcao ana wastani wa 0.90 katika michezo yote ya Ulaya. Cr7 yupo mbali sana na rekodi hii kwani ana wastani wa 0.68 ikikwa ni magoli 79 katika michezo 115. Messi yupo karibu sana na rekodi hii kwani ana wastani wa 0.80 ikiwa ni magoli 75 katika mechi 94. Inawezekana Messi na Ronaldo wakaifikia rekodi hii ya Gerd Muller ambayo imedumu kwa miongo kadhaa.
KUFUNGA MAGOLI MENGI KATIKA FAINALI YA ULAYA
Ferenc Puskas na Alfredo
Di Stefano wote wanashikilia rekodi ya kufunga mara nyingi katika fainali za Ulaya. Messi amefunga magoli mawili katika fainali mbili tofauti za mwaka 2009 na 2011. Ronaldo naye amefanya hivo mwaka 2008 na 2014. Puskas na Di Stefano wamefunga magoli 7 katika fainali, huku Puskas mwenyewe akifunga magoli 4 katika fainali moja ya Ulaya mwaka 1960. Kumbuka hawa wote ni magwiji wa Real Madrid. Ili Messi na Ronaldo waivunje hii rekodi wanapaswa kufunga magoli 5 kila mmoja katika fainali zijazo.!
KUFUNGA MAGOLI MENGI KATIKA HATUA YA MAKUNDI
Raul Gonzalez
Anashikilia rekodi ya kufunga magoli 53 katika hatua ya makundi kwenye michuano ya UEFA. Messi amejaribu kwa kufunga magoli 44 huku mpinzani wake Cr7 akifunga magoli 41 ukijumlisha na yale ya jana. Ukijaribu kutafakari utagundua hawa jamaa wapo karibu kuifika rekodi hii ambayo bado inashikiliwa na mkongwe kutoka ligi ya Hispania.
KUFUNGA MAGOLI MFULULIZO
Mholanzi Ruud Van Nistelrooy
 Alifunga magoli 9 mfululizo wakati akiwa Manchester United msimu wa 2002-3. Cr7 alikaribia kuifikia rekodi hii 2013-14 pale alipofunga magoli 8 mfululizo. Messi hajawahi kuikaribia rekodi hii licha ya kuwa bora duniani. utokana na Cr7 kuanza vyema inawezekana msimu huu akaifikia na kuvunja rekodi hii ya van Nisterooly ambayo imedumu kwa takribani miaka 13 sasa kwenye vitabu vya soka.
KUFUNGA HAT-TRICK YA MAPEMA ZAIDI
Magoli 3 aliyoyafunga Messi dhidi ya Arsenal mwaka 2011, ndiyo hat-trick yake ya mapema zaidi kwenye UEFA. Cristiano Ronaldo jana alipiga hat-trick ndani ya dakika 26 ila 2013 pia alipiga hat-trick ndani ya dakika 27 dhidi ya Galatasaray. Wanaume hawa wameshindwa kuifikia rekodi ya Bafetimbi Gomis ambaye alifunga hat-trick ya mapema zaidi kwenye UEFA (dakika 8) pale timu
yake ya zamani ya Olympic Lyon ilipokutana na Dinamo Zagreb. Rekodi hii Cr7 na Messi wanaitazama kwa jicho la karibu.
GOLI LA MAPEMA ZAIDI
Akiwa Bayern Munic, Roy Makaay alifunga goli ndani ya sekunde 10.12 pale timu yake ilipokutana na Real Madrid mwaka 2007. Wakati Messi goli lake la mapema zaidi kwenye UEFA ni lile alilowafunga FC Basel mwaka 2008, Cr7 naye aliwafunga Juventus mwezi October mwaka 2013 na kuwa goli la mapema ila wanandinga hawa wote wanaifukuzia rekodi ya Roy Makaay, rekodi ambayo inawezekana ni ngumu sana kwa sasa

Hakuna maoni: