VAN GAAL HANA SHAKA NA ROONEY, MAGOLI YAPO TU!
Rooney, mwenye Miaka 29, ndie Mfungaji Bora wa England na sasa anainyemelea Rekodi ya Ufungaji Bora Klabuni Manchester United inayoshikiliwa na Sir Bobby Charlton ya Mabao 249.
Kwenye Historia ya Ligi Kuu England, Alan Shearer ndio mwenye Rokodi ya Ufungaji Bao nyingi akiwa na Mabao 260 akifuatiwa na Andy Cole, aliewahi kuichezea Man United, aliefunga Bao 187 na Wayne Rooney anazo Bao 185.
Licha kuwa na ukame wa Mabao kwenye Ligi, Rooney alipiga Hetitriki hivi karibuni wakati Man United inaiinyuka Klabu ya Ubelgiji, Club Brugge, katika Mechi ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
++++++++++++++++++++++++
MAN UNITED
Wafungaji Bora:
-Sir Bobby Charlton: Mechi 758 Mabao 249
-Dennis Law Mechi 404 Mabao 237
-Wayne Rooney Mechi 484 Mabao 233
++++++++++++++++++++++++
Akiongea na Wanahabari hapo Jana kuhusu Mechi yao ya Ligi Kuu England ya Jumapili ya Ugenini na Southampton, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, ameeleza: “Sijali nani anafunga. Tunapaswa kufunga Bao nyingi zaidi. Ukitawala Mechi unapaswa kufunga Bao zaidi. Rooney anayo Magoli. Na pia Juan Mata, Memphis Depay, Anthony Martial, Marouane Fellaini. Rooney amefunga Bao nyingi Man United, anaikaribia Rekodi ya Klabu. Natumaini ataivunja Rekodi.”
Rooney alizikosa Mechi 2 za Man United zilizopita baada ya kuwa na maumivu Mguuni lakini sasa yupo fiti kucheza Mechi hii ya Jumapili..
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 19
1445 Chelsea v Arsenal
1700 Aston Villa v West Brom
1700 Bournemouth v Sunderland
1700 Newcastle v Watford
1700 Stoke v Leicester
1700 Swansea v Everton
1930 Man City v West Ham
Jumapili Septemba 20
1530 Tottenham v Crystal Palace
1800 Liverpool v Norwich
1800 Southampton v Man United
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni