tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

11 Mei 2016

EURO 2016: KIKOSI CHA ENGLAND KUTANGAZWA JUMATATU IJAYO!


HODGSON-ENGLANDMENEJA wa Roy Hodgson sasa atatangaza Kikosi cha Timu ya Taifa ya England Jumatatu ijayo kwa ajili ya Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, ambazo zitachezwa kuanzia Juni 10 huko Nchini France.
Awali Kikosi hicho kilikuwa kitangazwe Alhamisi hii na Hodgson na jopo lake la Makocha limeamua kusogeza mbele mpaka Jumatatu ili kutathmini Mechi za mwisho za Ligi Kuu England ambazo zitachezwa Jumapili ijayo.
Hivi sasa kuna wasiwasi mkubwa kwa England kuwakosa Wachezaji wao wa kawaida ambao ni Majeruhi ama wale ambao ndio kwanza wamerudi Viwanjani baada ya kuwa Majeruhi kwa kipindi.
Miongoni mwa hao ni Straika wa Arsenal Danny Welbeck ambae Majuzi aliumia Goti na haijajulina atakuwa nje kwa muda gani huku mwenzake wa Arsenal Jack Wilshere, ambae amekuwa nje karibu Msimu wote, akirejea na kucheza Mechi 2 akitokea Benchi.
Wengine kwenye Listi hiyo ni Beki wa Everton Phil Jagielka ambae yupo nje sasa kwa Wiki kadhaa akiuguza Musuli za Pajani na Kiungo wa Liverpool Jordan Henderson ambae ndio kwanza amerejea Mazoezini baada ya kuumia Goti Mwezi uliopita.
Wachezaji ambao wana hakika ya kuikosa EURO 2016 kutokana na kuumia ni Alex Oxlade-Chamberlain wa Arsenal alieumia Goti na Fulbeki wa Manchester United Luke Shaw ambae hajarejea Uwanjani tangu avunjike Mguu Mwezi Septemba.
Kikosi cha England kinatarajiwa kukusanyika kambini kwenye Kituo chao cha Mazoezi cha St George's Park Mei 18 kwa ajili ya matayarisho yao ya Mechi zao 3 za kujipima kabla ya EURO 2016.
Kwenye Mechi hizo, England itacheza na Turkey Uwanjani Etihad Jijini Manchester Jumapili Mei 22 na Siku 5 baadea kucheza na Australia huko Stadium of Light, Sunderland na kasha kutinga Wembley Stadium, London kuivaa Portugal hapo Alhamisi Juni 2.
Siku ya mwisho kwa Nchi washiriki wa Fainali za EURO 2016 kuwasilisha Majina ya Vikosi vyao vya Wachezaji 23 kwa UEFA watakaocheza Fainali hizo ni Jumanne Mei 31.

Hakuna maoni: