KIPIGO: VAN GAAL-KUSHAMBULIWA BASI SI KISINGIZIO, FA YACHUNGUZA PAMOJA NA DE GEA KUPIGWA CHUPA UWANJANI!
Wakielekea Uwanjani kabla ya Mechi hiyo ya kihistoria kwani ndio ilikuwa ya mwisho kabisa kwa West Ham kuchezea Uwanja wa Nyumbani Upton Park, Basi la Timu ya Man United lilipigwa Chupa na Makopo na kuvunjwa Vioo kadhaa.
Baada ya kipigo chao, Van Gaal alisema kulaumu kushambuliwa Basi lao ni kutafuta kisingizio lakini alikiri hilo pengine limeathiri Wachezaji wake chipukizi.
Van Gaal, mwenye Miaka 64, alisema: “Nina uzoefu mkubwa kwenye Soka na wapo Wachezaji hawana uzoefu huo.”
Hata hivyo, Van Gaal anaamini bado wana nafasi ya kufuzu 4 Bora wakiwafunga Bournemouth Jumapili Uwanjani Old Trafford kwani Wapinzani wao Man City wana Mechi ngumu ya Ugenini na Swansea City.
FA KUCHUNGUZA MASHAMBULIZI
WAKATI huo huo, FA, Chama cha Soka England, kinachunguza shambulizi la Basi la Man United pamoja na Kipa wao David De Gea kurushiwa vitu na Chupa wakati wa Mechi.
Kushambuliwa kwa Basi hilo kulisababisha Mechi hiyo ichelewe kuanza kwa Dakika 45.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni