tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

11 Mei 2016

La Liga: Miaka 23 ya kumbukumbu Mbaya Ya Siku Ya Mwisho Ya ligi Kwa Madrid – Wataandika Historia Mpya?




Real Madrid bado wana nafasi ya kushinda ubingwa wao wa 33 wa ligi siku tatu zijazo lakini wana kumbukumbu mbaya za kugombea ubingwa mpaka siku ya mwisho ya ligi.
  Mnamo msimu wa 1991/92, Real walikuwa pointi moja mbele ya Barcelona huku kukiwa na mechi moja ya kuchezwa.
Los Blancos’ ‘Dream Team’ iliyokuwa na wachezaji kama Fernando Hierro na Gheorghe Hagi walielekea Tenerife katika uwanja wa Estadio Heliodoro Rodriguez Lopez wakihitaji ushindi ili kushinda ubingwa wao 26 wa ligi.
Hierro na Hagi walianza kufunga kwa upande wa Madrid lakini mambo yakabadilika na balaa likahamia upande wa Los Blancos.
Barcelona wakaenda kushinda ubingwa baada ya kuwafunga Athletic Club 2-0 katika dimba la
Bernabeu baada ya Tenerife kurudi mchezoni na kuwafunga Real 3-2.
Kumbukumbu mbaya haishii hapo, historia ikajirudia na kuja kuwaandama tena Real Madrid msimu uliofuatia – walipocheza mechi ya mwisho tena na Tenerife.
Madrid wakafungwa 2-0 na Tenerife huku Barcelona wakishinda mechi ya mwisho na kubeba ubingwa wa pili mfululizo kwa tofauti ya pointi 1. Huu ulikuwa ubingwa wa 13 wa Barcelona.
  Miaka 23 baadae, jumamosi hii Real Madrid na FC Barcelona watacheza mechi zao za mwisho za La Liga huku Barca akiwa mbele kwa tofauti ya pointi 1, vijana wa Luis Enrique watacheza dhidi ya Granada ugenini na Real Madrid watacheza dhidi ya Deportivo. Historia mpya itaandikwa au mzimu wa matokeo mabaya utaendelea kuiandama Madrid katika siku ya mwisho ya ligi?

Hakuna maoni: