Pochetinno amfagilia Wanyama
Meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza Mauricio
Pochettino amemwagia sifa kiungo wa kati wa klabu hiyo raia wa Kenya
Victor Wanyama na kusema kuwa ni "mnyama".
Kocha huyo amesema mchezaji huyo ana sifa, nguvu na uwezo wa kuifaa sana klabu hiyo msimu huu.
"Ni mnyama, ninamfahamu vyema kwa sababu nilimnunua nikiwa Southampton kutoka Celtic. Ni rahisi sana kutambua sifa hizi," alisema Pochettino.
Wanyama alinunuliwa kwa pauni milioni 11 na Spurs kutoka Southampton mwezi Juni mwaka huu na kujiunga na kocha Ponchettino ambaye ndiye meneja aliyemnunua kutoka Celtic kwa pauni milioni 12.5 mwaka 2013.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni